2 Kings 4:42-44

42 aAkaja mtu kutoka Baal-Shalisha, akimletea mtu wa Mungu mikate ishirini ya shayiri iliyookwa kutokana na nafaka ya kwanza, pamoja na masuke ya nafaka mpya. Al-Yasa akasema, “Wape watu ili wale.”

43 bMtumishi wake akamuuliza, “Nitawezaje kuandaa hii mbele ya watu mia?”

Lakini Al-Yasa akajibu, “Wape watu ili wale. Kwa maana hivi ndivyo asemavyo Bwana: ‘Watakula na kusaza.’ ”
44Basi akaiandaa mbele yao ile mikate, wakala na baadhi yake wakasaza, sawasawa na neno la Bwana.
Copyright information for SwhKC